Magazeti leo Aprili 28,2026

Jumla ya watoto 252 wamepata huduma za upasuaji wa moyo kupitia ushirikiano uliopo kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel hatua iliyosaidia kuokoa maisha yao.
Kati ya watoto hao 170 walifanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu zilizofanywa hapa nchini na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa SACH huku watoto 82 wakipelekwa nchini Israel kwa matibabu zaidi.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI, Dkt. Naizihijwa Majani alipokuwa akizungumza na Balozi wa Israel nchini Tanzania Mhe. Gideon Behar alipotembelea taasisi hiyo kujionea huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na uwekezaji uliofanywa na serikali ya Tanzania katika matibabu ya moyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here