Waziri Kombo ateta na Balozi Mkingule,amhimiza kuimarisha mahusiano ya Tanzania na Cuba

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana kwa mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Cuba, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake ya kidiplomasia.
Akizungumza Aprili 27, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, Waziri Kombo amesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba.
Amemtaka Balozi Mkingule kutumia vyema uzoefu alioupata alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia ili kuongeza tija katika ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa upande wake, Balozi Mkingule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba.
Aidha, amemhakikishia Waziri Kombo kuwa atafanya kazi kwa bidii kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba kwa manufaa ya pande zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here