Waziri Makonda aitaka Bodi ya Ligi kuboresha usimamizi wa marefa

ARUSHA-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, Ameitaka Bodi ya Ligi na mamlaka husika kuweka mkazo kwenye maadili, nidhamu na weledi katika upangaji na usimamizi wa marefa ili kuhakikisha michezo inaendeshwa kwa haki na viwango vinavyokubalika kimataifa.
Waziri Makonda amesema hayo leo Aprili 30, 2026 katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo ameeleza kuwa licha ya ushindani mzuri uwanjani, bado kuna changamoto katika usimamizi wa marefa.

Amebainisha kuwa,vitendo hivyo vinasababisha mashabiki kupoteza imani na hata kufikia hatua ya kuwasifia marefa kutoka nje ya nchi.

Aidha, Waziri Makonda amewapongeza Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kufuatilia mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa Zanzibar, huku akisisitiza umuhimu wa kuboresha viwango vya uamuzi wa marefa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here