Jela miaka 30 kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi Mbarali

MBEYA-Mahakama ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Hilali Ngunguru mkazi wa Kijiji cha Miyombweni, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.
Mbali na adhabu hiyo, mahakama pia ilimhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari Miyombweni.

Aidha,aliamriwa kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa mhanga kutokana na madhara yaliyosababishwa na kitendo hicho.

Hukumu hiyo ilitolewa Mei 5, 2026 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbarali, Mhe. Nico Mwakibibi (SRM), baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka na kuthibitisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo.

Awali, upande wa mashtaka ulidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mwezi Desemba mwaka 2024 baada ya kumshawishi mwanafunzi huyo kuingia katika mahusiano ya kimapenzi yaliyosababisha ubakaji na ujauzito.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Faraja Langa aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo na kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoendelea kujitokeza katika jamii.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto vinaathiri ustawi, elimu na maisha ya baadaye ya watoto, hivyo kuna umuhimu wa jamii kushirikiana na vyombo vya dola katika kutoa taarifa mapema ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Mahakama ilisisitiza kuwa,sheria haitavumilia vitendo vya kuwadhulumu watoto na kwamba adhabu kali zitaendelea kutolewa kwa watakaobainika kujihusisha na makosa ya ukatili wa kijinsia, hususan dhidi ya wanafunzi na watoto walio chini ya ulinzi wa kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here