Magazeti leo Mei 10,2026

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Dorothy Gwajima, amezindua rasmi Mwongozo wa Kuratibu Ushiriki wa Wadau wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika Mikutano ya Kikanda na Kimataifa wa mwaka 2024, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na tija ya ushiriki wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa.
Akizungumza Mei 9,2026 jijini Dodoma wakati wa kikao cha wadau walioshiriki Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani (CSW70), Dkt. Gwajima amesema mwongozo huo umeandaliwa mahsusi kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji pamoja na tathmini ya ushiriki wa Serikali na wadau mbalimbali katika mikutano ya nje ya nchi.

Amesema hatua hiyo itawezesha Serikali kuwa na mfumo madhubuti wa kufahamu mikutano inayoshirikisha wadau wa maendeleo ya jamii, jinsia na wanawake, sambamba na kutathmini manufaa yanayopatikana kwa taifa kupitia ushiriki huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here