DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. William Samoei Ruto amewasili jijini Dodoma Mei 5, 2026 kuendelea na ziara yake ya kitaifa ya siku mbili hapa nchini.
Mhe. Rais William Ruto mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Rosemary Senyamule.Akiwa Dodoma, Mhe. Rais William Ruto atahutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais huyo kuhutubia Bunge hilo na ikiwa ni mara ya pili kutembelea Dodoma baada ya ziara yake ya mwaka 2022.
Aidha, baada ya shughuli hiyo Bungeni, Mhe. Rais William Ruto ataelekea Ikulu ya Rais iliyopo Chamwino ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.











