Tume ya Madini yatoa leseni zaidi ya 11,000 kwa Julai 2025 hadi Machi 2026

DODOMA-Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini katika kipindi cha Mwezi Julai 2025 hadi Machi 2026, ilifanikiwa kutoa jumla ya leseni 11,674 ikilinganishwa na lengo la kutoa leseni 11, 463.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Waziri Mavunde alilieleza Bunge kuwa, katika kipindi husika leseni zilizotolewa ni pamoja na Leseni ya Uchimbaji wa Kati wa Madini (MLs) 21, Leseni zacUtafutaji wa Madini (PLs) 313, Leseni za Uchimbaji Mdogo (PMLs) 8,878, Leseni za Uchenjuaji Madini (PCLs) 41, Leseni za Biashara Kubwa ya Madini(DLs) 914 na Leseni za Biashara ndogo ya Madini ( (BLs) 1507.

Akielezea leseni zilizoshindwa kukidhi matakwa ya kisheria , Waziri Mavunde alifafanua kuwa, leseni 111 za utafutaji wa madini na leseni 35 za uchimbaji wa Kati wa madini zilipewa hati za makosa kutokana na kutolipa ada za mwaka na kutoendeleza maeneo ya leseni.

Aidhaleseni 53 za utafutaji madini na leseni 29 za uchimbaji wa kati wa madini zilifutwa baada ya wamiliki wake kushindwa kurekebisha makosa yao.

Waziri Mavunde aliongeza kuwa , katika kipindi husika jumla ya mitambo 52 ya kuchenjua dhahabu (CIP /CIL), Vat Leaching 509 na Elution 204 zilikaguliwa katika Mikoa ya Kimadini 25.

Kwa upande wa ufungaji migodi , mipango ya ufungaji migodi minne ilijadiliwa na Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi kati ya mipango hiyo, hakuna mpango ulioidhinishwa kutokana na kubainika kwa mapungufu mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa taarifa za utafiti wa uimara wa miamba pamoja na kukosekana kwa maoni ya wadau wa Kamati ya Wilaya ya Ufungaji Migodi ili kainisha miradi ya kiuchumi kwa jamii baada ya kufungwa kwa migodi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here