Wizara ya Fedha yaendelea na mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma sura ya 410 kuendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

NA SAIDINA MSANGI
WF

WIZARA ya Fedha inaendelea na mchakato wa kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kupitia kikao kazi kilichowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi.
Kaimu Kamishna, Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Alex Haraba, akizungumza wakati akifungua kikao kazi kilichokutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kufanya mapitio ya kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya St. Gasper, jijini Dodoma.

Mchakato huo umeanza kwa kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper jijini Dodoma, ambapo wadau walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha Sheria hiyo.

Akifungua kikao hicho, Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Alex J. Haraba, alisema mapitio hayo yanalenga kujenga mfumo wa kisasa unaojumuisha hatua zote za mnyororo wa ugavi, kuanzia upangaji wa mahitaji, ununuzi, upokeaji na ugomboaji, uhifadhi na utunzaji, usambazaji, hadi uondoshaji wa mali.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi Emma Komba, akichangia hoja katika kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya St. Gasper, jijini Dodoma.

‘‘Mapitio ya sheria hii ni hatua ya kimkakati ya kuhakikisha kuwa masuala yote yanayohusu mnyororo mzima wa ugavi yanajumuishwa kikamilifu katika Sheria mpya, na kwamba mageuzi hayo yatakuwa chachu ya kuchochea maendeleo ya Taifa kwa kuzingatia nguzo na malengo ya Dira ya Maendeleo 2050, ikiwemo ukuaji wa uchumi, maendeleo ya viwanda, pamoja na maendeleo jumuishi na endelevu,’’ alisema Bw. Haraba.

Aliongeza kuwa Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, imeipa Wizara ya Fedha jukumu la kisheria la kupitia na kuhuisha sera, sheria, kanuni, miongozo, pamoja na maelekezo mbalimbali yanayohusu ununuzi wa umma na ugavi nchini.
Meneja Msaidizi, Tenda na Mikataba kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Magnus Mlokota, akitoa maoni katika kikao kazi cha kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya St. Gasper, jijini Dodoma.

Bw. Haraba alifafanua kuwa maoni yote yatakayowasilishwa yatachambuliwa kwa kina ili kubaini maeneo ya kuboresha na kuweka misingi imara itakayosaidia Taifa kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo 2050.

Aidha, Bw. Haraba aliwahimiza wadau kushiriki kikamilifu kutoa maoni na kukisisitiza kuwa ushiriki wao ndio utakaohakikisha Sheria mpya inakuwa bora, jumuishi na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.

Aliongeza kuwa Wizara ya Fedha itazingatia na kufanyia kazi mapendekezo yote yatakayowasilishwa katika hatua zinazofuata za mapitio hayo.ni Dodoma.
Baadhi ya wadau wakishiriki hoja zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao kazi cha kupitia upya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya St. Gasper, jijini Dodoma.

Kikao hicho, kilichoratibiwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, kiliwakutanisha pamoja wadau mbalimbali kutoka Sekta ya umma na binafsi.

Kwa upande wa sekta ya umma, taasisi zilizoshiriki ni pamoja na Tume ya Mipango, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wakala wa Majengo (TBA), Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), pamoja na Bodi ya Usajili wa Wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB).
Kaimu Kamishna, Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bw. Alex Haraba, akiwa katika picha ya pamoja na wadau baaada ya kuhitimisha katika kikao kazi cha kufanya mapitio ya Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura ya 410, kwa lengo la kuioanisha na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya St. Gasper, jijini Dodoma. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi Emma Komba na kushoto ni aliyekuwa Katibu wa Kikao kazi hicho ambaye ni Mwanasheria kutoka Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bw. Paul Kimweri.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Kwa upande wa sekta binafsi, walishiriki wazabuni mbalimbali wakiwemo Jali Motors Ltd, Firebrand Technologies, Primezone Ltd, Mr. Jumbo, Dynatech Solution Ltd, Vera International Travelling Agency, New Jari Fashion Ltd na Blueberry Travel, ambao walipata fursa ya kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuboresha mazingira ya biashara na ushiriki wao katika shughuli za ununuzi wa umma na ugavi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here