Diplomasia,amani na utulivu vimeendelea kuvutia mikutano ya Kimataifa nchini-Naibu Waziri Millya

ARUSHA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Mhe. James Millya amesema Diplomasia ya Tanzania imeendelea kuimarika duniani katika Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Millya alitoa kauli hiyo jijini Arusha Juni 29, 2026 kufuatia uamuzi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Warsha ya Nne ya Kimataifa ya masuala ya Utabiri wa Hali ya Hewa kwa Uendeshaji (The Fourth WMO International Workshop on Operational Climate Prediction - OCP4).

Mhe. Millya alieleza kuwa Warsha hiyo iliyoanza Juni 29 jijini Arusha na itahitimishwa Julai 03, 2026 ni mara ya kwanza kufanyika barani Afrika na nchi nyingine zilizowahi kuwa mwenyeji wa warsha hiyo ni Ureno, Hispania na India.
"Nchi hizi mbili ni za Ulaya na moja ni ya Asia, hivyo sisi kama Tanzania kuwa mwenyeji wa warsha hii ni jambo la kujivunia na halikuja kwa bahati mbaya isipokuwa mikakati imara ya kidiplomasia,"Mhe. Millya alisema.

Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania imeimarika katika nyanja ya usalama, diplomasia, miundombinu na kuwa na uzoefu na uwezo mkubwa wa kuandaa matukio makubwa kama haya ni moja ya vigezo iliyosababisha kuchaguliwa na WMO.
Aidha, kuimarika kwa huduma na miundombinu ya utabiri wa hali ya hewa nchini na kuwa na wataalam wabobevu ambao baadhi yao wanatumika na WMO katika nafasi mbalimbali pamoja na kutoa misaada ya kiufundi katika nchi marafiki kama vile Sudan Kusini, Maldives na Namibia vimeiweka Tanzania katika sura nzuri kimataifa.

Alimalizia kwa kueleza kuwa mkutano huo ambao nchi zaidi ya 20 zinashiriki ni fursa ya kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla na kuwasihii waendele kudumisha amani ili iendelee kuja nchini.
Wataalam wa fani mbalimbali wanashiriki warsha hiyo ambayo imejikita zaidi katika kuimarisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utabiri wa hali ya hewa utakaotoa taarifa sahihi na kutafsiriwa kwa wakati ili kuleta tija katika sekta za kilimo, usafiri, maji na udhibiti wa majanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here