NA DIRAMAKINI
KATIKA mchezo wa ufunguzi wa Kundi husika la michuano ya Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kuondoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ecuador.
Ni katika mchezo ulioshuhudiwa ukiwa na ushindani mkali ambao uliovuta hisia za mashabiki wengi dimba la Philadelphia lililopo mjini humo nchini Marekani.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa katika dakika ya 90 kupitia mshambuliaji Amad Diallo, ambaye alitumia vyema nafasi iliyopatikana na kuipatia timu yake pointi tatu muhimu za awali katika kampeni ya mashindano hayo makubwa duniani.
Ecuador walionekana kujituma na kushambulia kwa nguvu, wakisukumwa zaidi na ushangiliaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wao waliojazana uwanjani.
Hata hivyo, juhudi zao ziligonga ukuta imara wa ulinzi wa Ivory Coast, uliodumu hadi filimbi ya mwisho.
Kipindi chote cha mchezo kilishuhudia kasi, mabadiliko ya kimkakati na ushindani mkali katikati ya uwanja, lakini Ivory Coast walifanikiwa kudhibiti mchezo na kulinda uongozi wao hadi dakika 90 kukamilika.
Kwa ushindi huo, Ivory Coast wanaanza vyema safari yao ya Kombe la Dunia, huku Ecuador wakitakiwa kujipanga upya katika michezo ijayo ili kurejesha matumaini ya kusonga mbele.
