Polisi wamsaka dereva aliyehusika kwenye ajali Moshi Mjini jana

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamsaka mtu mmoja aliyekuwa dereva wa gari lenye namba za usajili T. 488 DMN aina ya Mitsubishi Canter mali ya Luchmen Suleiman Msoffe baada ya kusababisha ajali iliyopelekea majeruhi watatu eneo la barabara ya kuelekea soko la Manyema Moshi mjini Juni 27, 2026.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Simon Maigwa.

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili asubuhi gari hiyo ikitokea uelekeo wa msikiti wa Riadha Moshi mjini kuelekea soko la Manyema ambapo gari hiyo ilipoteza uelekeo na kugonga vibanda vya biashara na watembea kwa miguu na kupeleka uharibifu wa mali na majeruhi kwa watu watatu.

Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Sikudhani Nuru Msangi (38) mkazi wa Mabogini na mfanyabiashara, Elinipa Aimbingi Matemba (75) mkazi wa Majengo na Daniel Lazaro Lemeru (37) mkazi wa Arusha.

Majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa,chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kuchukua tahadhari kwenye eneo lenye mkusanyiko wa watu na watumiaji wengine wa barabara ambapo alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linaishikilia gari hiyo ikiwa ni pamoja na kumtafuta mmiliki wake na Dereva huyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here