Timu ya wataalamu Ofisi ya Rais-Utumishi na Watumishi Housing Investments (WHI) yaendelea na ukaguzi wa utekelezaji miradi

LINDI-Timu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments (WHI) imeendelea na ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za Watumishi katika Mkoa wa Lindi ambapo Juni 27, 2026 imekagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za Watumishi katika Kituo cha Afya Hoteli Tatu, Shule ya Sekondari Matanda, Shule ya Msingi Runyu, Kituo cha Afya Mvuleni na Shule ya Sekondari Mvuleni.Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikikagua ubora wa kazi za ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Kituo cha Afya Hoteli Tatu, Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi tarehe 27 Juni 2026.
Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma la Kituo cha Afya Hoteli tatu kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi.


Timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora na Watumishi Housing Investments ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Patrick Allute kukagua mradi wa maendeleo wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mvuleni kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi.

Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma wa shule ya sekondari Mvuleni kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Patrick Allute akijadili jambo na Wataalamu kutoka Ofisi hiyo na Watumishi Housing Investments (WHI) mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Shule ya Sekondari Mvuleni iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Mkoa wa Lindi.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Patrick Allute (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu kutoka Ofisi hiyo na Watumishi Housing Investment mara baada ya kukamilisha ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya Watumishi katika Kituo cha Afya Hoteli Tatu, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here