Taarifa kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu kusimama kwa huduma za Treni kutokana na hitilafu katika mfumo wa Gridi ya Taifa leo Juni 27,2026

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kusimama kwa huduma za treni za Reli ya Kisasa (SGR) kutokana na hitilafu iliyotokea katika mfumo wa Gridi ya Umeme ya Taifa.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Juni 27, 2026 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa TRC, Fredy Mwanjala ni kwamba shirika hilo limewaomba radhi abiria wote walioathirika na usumbufu uliojitokeza kutokana na kusimama kwa huduma hizo.

TRC imesema wataalamu wake kwa kushirikiana na wataalamu wa TANESCO wanaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kurejesha huduma za treni haraka iwezekanavyo.

Shirika hilo limewahakikishia Wananchi kuwa jitihada zinaendelea kuhakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida mara tu hitilafu hiyo itakapopatiwa ufumbuzi.

Taarifa ya TRC inakuja baada ya TANESCO kutangaza hitilafu ya umeme katika gridi ya Taifa iliyotokea jioni ya leo Juni 27, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here