Tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa walioomba nafasi za ajira Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)

DODOMA-Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa anawatangazia waombaji wote wa ajira waliofanya mtihani wa kuandika kutembelea akaunti zao za maombi ya ajira kupitia mfumo wa ajira wa TAKUKURU "https://ajira.pccb.go.tz" na kwa barua pepe zao ili kupokea taarifa na maelekezo ya tarehe, muda na eneo la kufanyia usaili wa ana kwa ana (Oral Interview) kwa waliofaulu

Mambo muhimu ya kuzingatia: -

1. Kila aliyeitwa kwenye usaili anatakiwa kufika kwa siku na muda aliopangiwa akiwa na nyaraka zifuatazo: -

1.1. Nakala halisi za vyeti vya masomo (Taaluma na kozi mbalimbali)

1.2. Picha tatu "Passport Size"

1.3. Nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa

1.4. Kitambulisho cha taifa (NIDA)

1.5. Majina ya wadhamini wawili, anwani zao na namba za simu.

2. Kuwasilisha nyaraka za kugushi ni kosa la Jinai

3. Kila atakayefika kwenye usaili huu anapaswa kujigharamia

Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
1 Mtaa wa TAKUKURU,
S.L.P. 129,
41101 DODOMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here