Tanzania yasisitiza mshikamano katika kushughulikia changamoto za Kikanda

DAR-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza utayari wake wa kuendelea kuunga mkono juhudi za kikanda za kuimarisha amani na usalama katika ukanda wa SADC wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 22 Juni 2026.
Akizungumza katika kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu kutokea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema, Tanzania inaunga mkono na kupongeza juhudi za upatanishi zinazoendelea kufanywa na SADC katika kanda na kueleza utayari wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Nchi Wanachama wa SADC katika juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama kwenye kanda.
Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC inaundwa na Nchi za Malawi Mwenyekiti, Eswatini Mwenyekiti ajaye na Tanzania Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ina jukumu la kulinda kusimamia na kuhakikisha amani, usalama na utulivu unatamalaki katika ukanda wa SADC.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza dhamira ya kuendelea kuimarisha amani na usalama katika ukanda wa SADC wakati wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 22 Juni 2026.
Akizungumza katika kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu kutokea katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, amesema Tanzania inaunga mkono na kupongeza juhudi za upatanishi zinazoendelea kufanywa na SADC katika kanda na kueleza utayari wa Tanzania kuendelea kushirikiana na Nchi Wanachama wa SADC katika juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama kwenye kanda.

Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC inaundwa na Nchi za Malawi Mwenyekiti, Eswatini Mwenyekiti ajaye na Tanzania Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ina jukumu la kulinda kusimamia na kuhakikisha amani, usalama na utulivu unatamalaki katika ukanda wa SADC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here