Dkt.Ngwaru Maghembe ashiriki Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa SADC ORGAN TROIKA

DAR-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe (Mb), ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) uliofanyika kwa njia ya mtandao kujadili hali ya usalama katika kanda.
Akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Maghembe aliipongeza SADC kwa juhudi za kuimarisha amani, usalama na kusuluhisha migogoro inayoibuka katika kanda.
Aidha, alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za SADC katika kuimarisha amani kwenye ukanda huo.

Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC inaundwa na Nchi za Malawi Mwenyekiti, Eswatini Mwenyekiti ajaye na Tanzania Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ina jukumu la kulinda kusimamia na kuhakikisha amani, usalama na utulivu unatamalaki katika ukanda wa SADC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here