Timu ya Ofisi ya Rais-Utumishi yakagua miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi Dodoma

NA ANTONIA MBWAMBO

TIMU ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais–UTUMISHI kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investment imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi awamu ya pili katika Wilaya ya Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na ratiba iliyopangwa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akitaka ufafanuzi wa jambo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kituo cha Afya kilichopo mtaa wa Hospitali kata ya Mkonze Mkoani Dodoma Juni 24,2025.

Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute, ambaye amesema Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya kazi na makazi ya watumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bw. Allute amesisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi, matumizi sahihi ya rasilimali za umma na ukamilishaji wa kazi kwa wakati huku viwango vya ubora vikizingatiwa.
Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma lililopo mtaa wa Hombolo senta, kata ya Hombolo,Wilaya ya Dodoma Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Wataalamu aliofuatana nao mbele ya jengo la Mradi wa shule ya sekondari Bihawana uliopo Mkonze jijini Dodoma mara baada ya kukagua maendeleo ya Mradi huo Juni 24, 2026.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (wa tatu kutoka kulia) akizungumza na Mwalimu ambaye ni Mtumishi katika shule ya sekondari Bihawana, Mkonze mara baada ya Mkurugenzi huyo na timu ta Wataalamu aliofuatana nao kuwasili katika mradi huo kwa ukaguzi Juni 25, 2026 jijini Dodoma.

Aidha, ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi na wakandarasi kushughulikia kwa haraka changamoto zilizobainika ili kuhakikisha malengo ya miradi hiyo yanafikiwa kama ilivyopangwa.

Ziara hiyo imekuwa sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha uwekezaji unaofanywa unaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyesimama katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya wataalamu wa ukaguzi wa miradi mara baada ya timu hiyo kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Watumishi katika kituo cha Afya Mkonze , mtaa wa hospitali Mkoani Dodoma.
Muonekano wa mbele wa jengo la mradi wa makazi ya Watumishi wa Umma lililopo katika Kijiji cha hospitali, kata ya Mkonze,Wilaya ya Dodoma na Mkoa wa Dodoma.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Patrick Allute (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa shule ya sekondari Mtemichiloloma Hombolo, Mkonze mara baada ya Mkurugenzi huyo na timu ta Wataalamu aliofuatana nao kuwasili katika mradi huo kwa ukaguzi Juni 25, 2026 jijini Dodoma.

Katika ukaguzi huo, timu imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika Kituo cha Afya Hombolo, Shule ya Sekondari Mtemichiloloma, Kituo cha Afya Mkonze na Shule ya Sekondari Bihawana, ambapo imejionea maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na imefanya majadiliano na wasimamizi pamoja na wakandarasi kuhusu hatua zilizofikiwa na changamoto zinazojitokeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here