Aliyekuwa Mwalimu Mkuu na Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Kitwai A wilayani Simanjiro hatiani kwa makosa ya uhujumu uchumi

NA DIRAMAKINI

JULAI 2,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi,Mheshimiwa Charles Uisso imetolewa hukumu katika shauri la uhujumu uchumi namba 12761/2026 dhidi ya aliyekuwa mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kitwai A,Bw. Simon Mhando Mungay na Bw. Petro Orkeli Long’owaji aliyekuwa mjumbe wa kamati ya shule.
Hapo awali washtakiwa walishtakiwa kwa makosa ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22, kusaidia kutendeka uhalifu kinyume na kifungu cha 30 vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Cap 329 R:E 2023 vikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza kifunhu cha 57(1) na 61(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Kupanga Cap 200 R: E , pamoja na makosa ya kugushi kinyume na kifungu cha 333, 335(a) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Cap 16 R:E 2023.

Washtakiwa walifanya makosa hayo kwa kuandaa hati nane za malipo ambazo zilikuwa na maelezo ya uongo kisha mshtakiwa namba moja akawasilisha nyaraka hizo ofisi ya DED Simanjiro kumwaminisha kuwa,ziliandaliwa na kusainiwa na mwalimu wa kamati ya fedha, kisha kupitia nyaraka hizo zenye maelezo ya uongo ofisi ya DED ikaidhinisha malipo ya jumla ya shilingi 800,000 kutoka fedha za CAPITATION za Shule ya Msingi Kitwai "A" kwenda kwa mshtakiwa namba moja.

Washtakiwa wote wawili wametiwa hatiani baada ya kufanya ple bargaining ambapo wamepewa adhabu ya kulipa shilingi 800,000 kwa mhanga ambaye ni Shuleya Msingi Kitwai "A" pamoja na kutumikia adhabu ya kifungo cha nje cha miezi sita.

Kwa sasa washtakiwa wote wawili wameshatekeleza adhabu ya kulipa shilingi 800,000 na wanaendelea kutumikia kifungo cha nje cha miezi sita.

Shauri hilo lilikuwa linaendeshwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU),Wakili Faustine Mushi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here