NA DIRAMAKINI
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza itaendesha minada ya Dhamana za Serikali za Muda Mfupi za siku 35, 91, 182 na 364, pamoja na za Muda Mrefu za miaka 2, 5, 10, 15, 20 na 25 kwa niaba ya Serikali.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma Julai 1,2026 ambayo imefafanua kuwa, minada hiyo itafanyika kuanzia Julai hadi Septemba,2026 kwa mpangilio ulioainishwa kwenye kalenda.Aidha,kiwango cha riba cha Hatibondani pamoja na taarifa nyingine za dhamana husika zitatangazwa kwenye tangazo la mnada (Call for Tender).
Pia,Minada ya Dhamana za Serikali itafanyika kwa mpangilio ulioainishwa, isipokuwa itakapotangazwa vinginevyo.
Vilevile,Serikali itafanya marekebisho katika kalenda ya utoaji wa dhamana endapo itahitajika, kulingana na mahitaji ya kukopa na mwenendo wa hali ya soko.