NA DIRAMAKINI
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa leseni ya benki kwa LOLC Tanzania Microfinance Bank Limited.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 1,2026 na Naibu Gavana wa BoT anayesimamia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha,Bi.Sauda K.Msemo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,leseni hiyo inairuhusu benki hiyo kufanya biashara za kibenki kama benki ya huduma ndogo za fedha (microfinance bank) kuanzia tarehe 11 Juni, 2026.
Aidha,Makao Makuu ya benki yapo katika Kiwanja Na.11, Kitalu 45A, ghorofa ya kati (mezzanine) na ghorofa ya kwanza ya jengo la Derm Complex lililopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

