DAR-Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jumanne Muliro, ametembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 6 Julai, 2026.
Katika ziara hiyo, SACP Muliro ameipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuweza kushiriki Maonesho ya Sabasaba na kuweza kusogeza huduma ya Ushauri wa Kisheria kwa Wananchi.Aidha, SACP Muliro amesisitiza uwepo wa amani na kutoa matumaini kwa wananchi juu ya hali ya Usalama, akibainisha kuwa vyombo vya dola vimejipanga kuhakikisha kila mwananchi anashiriki Maonesho ya Saba Saba bila hofu.
Wananchi wanaendelea kupata huduma ya Ushauri wa Kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia maonesho ya sabasaba yaliyoanza tarehe 28 Juni, 2026 yanaendelea hadi tarehe 13 Julai, 2026, ambapo banda la Ofisi liko katika Ukumbi wa Karume kwenye Viwanja vya SabaSaba Jijini, Dar es salaam.