Mfumo wa SCADA waimarisha ufanisi katika shughuli za ushushaji mafuta na kudhibiti upotevu

DAR-Mfumo wa kufuatilia, kudhibiti na kukusanya taarifa za mafuta yanayoingia nchini kwa wakati halisi (Supervisory Control and Data Acquisition -SCADA) umeendelea kuwa nyenzo muhimu katika kuimarisha usimamizi wa mafuta nchini kwa kuongeza uwazi, usahihi wa taarifa na ufanisi katika ushushwaji wa mafuta yanayoingia kupitia bandari zetu hadi kufika kwenye maghala ya kuhifadhia.
Kupitia mfumo huo, Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) umefanikiwa kuimarisha udhibiti wa upotevu wa mafuta na kuongeza uhakika wa takwimu zinazotumika katika kufanya maamuzi ya kiutendaji.
Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Afisa Lojistiki wa Mafuta wa PBPA, Bi. Hilda Kowero, alisema mfumo wa SCADA umeleta maboresho makubwa katika usimamizi wa mafuta kwa kuwezesha ufuatiliaji wa shughuli zote muhimu kwa wakati halisi.

"Teknolojia hii inatuwezesha kupata taarifa sahihi kwa wakati kuhusu mwenendo wa mafuta yanayoingia nchini. Hivyo, tunakuwa na uwezo wa kufuatilia mnyororo mzima kwa usahihi na kuongeza uwajibikaji katika usimamizi wa mafuta," alisema Bi. Kowero.
Aliongeza kuwa pamoja na kuratibu uagizaji wa mafuta kupitia Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Bulk Procurement System - BPS), PBPA pia ina jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na akiba na upatikanaji wa mafuta unaoaminika wakati wote hivyo kuimarisha usalama wa hali ya upatakinaji wa mafuta nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here