NA VERONICA MWAFISI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua tafiti tumizi sita zitakazokifanya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kuwa kitovu cha maarifa na ushahidi wa kisayansi kwa ajili ya kuboresha Utumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akibonyeza kitufe wakati akizindua tafiti tumizi sita wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) zitakazokifanya Chuo hicho kuwa kitovu cha maarifa na ushahidi wa kisayansi kwa ajili ya kuboresha Utumishi wa Umma.
Akizungumza katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Waziri Kikwete amesema Serikali inahitaji tafiti zitakazotoa suluhisho kwa changamoto halisi zinazokabili taasisi za umma.
Viongozi mbalimbali, Wadau na Wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakipiga makofi baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kuzindua tafiti tumizi sita wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo Jijini Dar es Salaam.
“Tunahitaji tafiti zinatakazosaidia kufanya maamuzi sahihi ya sera, kuboresha mifumo ya kazi, na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi,"amesema Mhe. Kikwete.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza baada ya kuzindua tafiti tumizi sita wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa ofisi yake, Bw. Juma Mkomi (kulia) baada ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kukabidhiwa Tuzo ya Utambuzi iliyotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kilichopo jijini Dar es Salaam.
Aidha, Waziri Kikwete amewapongeza watafiti wote walioshiriki katika kazi ya utafiti na kutoa rai kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Vyuo Vikuu na taasisi nyingine ili tafiti zake ziwe na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akielekea katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Florens Turuka na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Ernest Mabonesho.Waziri Kikwete ameongeza kuwa, anaamini miaka 25 ijayo itakuwa kipindi cha mafanikio makubwa zaidi, ambapo Chuo hicho kitaendelea kuwa kinara wa maendeleo ya rasilimali watu, tafiti tumizi, na ushauri wa kitaalamu kwa ajili ya kuimarisha Utumishi wa Umma na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


