Polisi watoa ufafanuzi kuhusianiana tukio la mtu mmoja kufariki dunia Ngorongoro

ARUSHA-Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema kuwa lilipokea taarifa kuwa kuna watu wawili wanaume wamefikishwa katika Hospitali ya Lutheran wilayani Karatu na kati ya hao wawili mmoja alikuwa ameshafariki dunia na mmoja alikuwa hai anaendelea kupatiwa matibabu.
Akifafanua tukio hilo leo Agosti 13, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema, mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Askari Polisi walifika katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo na kama kimesababishwa na mtu ni nani au watu gani wamehusika na katika mazingira gani.

SACP Masejo amesema uchunguzi wa awali ulibaini aliyekuwa amefikishwa hospitalini akiwa amefariki anaitwa Sefu Mussa (25) fundi gereji mkazi wa Matejo jijini Arusha.

Ameendelea kufafanua kuwa, mtu wa pili ambaye alikuwa anaendelea kupatiwa matibabu alitambulika kwa jina la Salimu Haji maarufu Chambega, Fundi Gereji na Mkazi wa Makao Mapya jijini Arusha.

Aidha, amesema uchunguzi zaidi ulifanikisha kupata taarifa kuwa, watu hawa wawili pia walikuwa na mtu mwingine anayejulikana kwa jina la Abdallah Nuru maarufu Ngandana, Fundi Gereji Mkazi wa Matejo Arusha ambaye inadaiwa ndiye alikuwa anaendesha pikipiki iliyokuwa imewabeba wote watatu.

Ameendekea kufafanua kuwa inadaiwa watu hao kwa pamoja Agosti 12, 2026 muda saa nne asubuhi walikamatwa na Askari wa Uhifadhi Ngorongoro baada ya kuingia kwenye eneo hilo bila kufuata utaratibu na wakiwa na pikipiki ambazo haziruhusiwi kuingia katika hifadhi hiyo.

Kamanda Masejo ameendelea kueleza kuwa, inadaiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa walieleza walikuwa wametokea jijini Arusha wakiwa na pikipiki kuelekea Babati kwenye msiba na wakapotea njia wakajikuta wapo kwenye hifadhi ya ngorongoro.

Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linaendelea na Uchunguzi zaidi wa kuthibitisha taarifa hizo za awali, kwani limeshapa maelezo ya baadhi ya watu ili kusaidia kupata ukweli wa nini kilitokea baada ya kukamatwa na Askari hadi mmoja kufariki dunia na mwingine kuendelea kupatiwa matatibu hospitalini na wa tatu kufanikiwa kurejea jijini Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here