Magazeti leo Septemba 30,2026

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameagiza kusitishwa kwa utekelezaji wa mfumo wa pointi kwa madereva, akisema mfumo huo ulikuwa bado haujaanza kutekelezwa rasmi na ulikuwa katika hatua ya majaribio.
Katambi ametoa agizo hilo Septemba 29, 2026, katika Stendi ya Kimataifa ya Magufuli jijini Dar es Salaam, alipokutana na madereva kufuatia mgomo ulioanza asubuhi ya jana.

Amesema uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa kufanyika kwa tathmini ya kina ya mfumo huo, huku madereva na viongozi wao wakishirikishwa katika mchakato huo.

“Kwa hiyo mpaka sasa ninavyozungumza kwenye jambo hili la pointi, maagizo na maelekezo yangu na uamuzi wangu ni huu, jambo hili lisitishwe na tathmini ya kina itafanyika kwa kuwashirikisha madereva hawa wote kupitia viongozi wao, kuanzia viongozi wa wamiliki,” amesema Katambi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here