Nje Sports yatinga 16 bora SHIMIWI 2026

KILIMANJARO-Timu ya Netiboli ya Wanawake ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (NJE Sports) imehitimisha hatua ya makundi ya Mashindano ya SHIMIWI 2026 ikiwa na pointi tisa na kufuzu hatua ya 16 bora.
NJE Sports imekamilisha hatua hiyo kwa mchezo dhidi ya Mahakama uliopigwa katika Uwanja wa Moshi Club mkoani Kilimanjaro, na kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake nyuma ya Mahakama.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha wa NJE Sports, Mathew Kambona, amesema kufuzu hatua ya 16 bora ni matokeo ya juhudi na nidhamu ya wachezaji licha ya changamoto ya majeruhi ndani ya kikosi.
"Tumemaliza tukiwa na pointi tisa na tumeshika nafasi ya pili nyuma ya Mahakama. Wachezaji wamepambana na kufuata maelekezo ya kiufundi, na sasa tunasubiri kujua tutakutana na nani hatua ya 16 bora,” amesema Kambona.

Akitoa tathmini ya hatua ya makundi, Kambona amesema kundi hilo lilikuwa gumu kutokana na ushindani kutoka kwa Mahakama na RAS Mwanza, huku akisisitiza kuwa kufuzu ni matokeo ya kazi kubwa ya kikosi pamoja na sapoti kutoka kwa viongozi wa Wizara.
NJE Sports sasa inaelekeza nguvu katika maandalizi ya hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here