ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 28,2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mji wa Michezo Zanzibar (AFCON), Fumba Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja.
Rais Dkt.Mwinyi amekagua miundombinu mbalimbali ikiwemo uwanja wa mpira wa miguu, viwanja vya mazoezi, mabwawa ya kuogelea na Diving Pool, Fan Zone yenye uwezo wa watu 4,000, pamoja na bandari kwa ajili ya boti ndogo na kubwa.
Awamu ya kwanza ya mradi inatarajiwa kukamilika Desemba 31, 2026 ikiwa ni hatua muhimu kuelekea Zanzibar kuwa miongoni mwa wenyeji wa mashindano ya AFCON.










