Magazeti leo Septemba 22,2026

Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imebainika kuwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na mafuriko kwa kiwango cha asilimia 75, huku Mkoa wa Pwani ukikadiria zaidi ya Sh bilioni 32.6 zitahitajika kwa ajili ya maandalizi na kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba mwaka huu hadi Januari 2027.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema kati ya fedha hizo, takribani Sh bilioni 17 zinahitajika kwa ajili ya Wilaya ya Rufiji, ambayo imekuwa ikikumbwa na mafuriko kutokana na historia na jiografia yake, ikiwemo athari zilizojitokeza katika msimu wa mvua wa mwaka 2023/2024.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa maendeleo, wakiwemo wawekezaji na viongozi mbalimbali mkoani Pwani, Nyongo amesema pamoja na Rufiji, maeneo mengine ni Bagamoyo, Kibiti na Kisiwa cha Mafia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here