ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameungana na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza ya Marehemu Burhan Mohammed, baba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA),ndugu Juma Burhan Mohamed.
Sala hiyo ya Jeneza imesaliwa leo Septemba 25,2026 katika Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja.
Baada ya Sala ya Jeneza, Rais Dkt. Mwinyi ameungana na wanafamilia, waumini na wananchi kuusindikiza mwili wa marehemu Burhan Mohammed katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja, ambako amezikwa.
Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.








