Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yatunukiwa Tuzo katika Jukwaa la Fungua Fursa

GEITA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetunukiwa tuzo maalum katika Jukwaa la Fungua Fursa mkoani Geita, ikiwa ni kutambua mchango wa ofisi katika utoaji wa huduma za elimu na ushauri wa kisheria nchini na kwa wananchi na washiriki wa Maonesho ya Kitaifa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita.
Tuzo hiyo imetolewa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) leo Septemba 25, 2026 na kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mhe. Hashim Abdallah Komba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Mheshimiwa Alexander Mnyeti.

Aidha,tuzo hiyo imepokelewa na Wakili wa Serikali Mkoa wa Kagera Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Richard Nkaina.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inashiriki katika Jukwaa la Fungua Fursa Mkoa wa Geita kwa kutoa elimu na ushauri wa kisheria kwa wananchi wa mkoa huo.
Uzinduzi rasmi wa Jukwaa la Fungua Fursa unafuatiwa na Maonesho ya Kitaifa ya Madini yalioanza Septemba 23, 2026 na yataendelea hadi Oktoba 3,2026 katika Viwanja vya Maonesho vya Dkt.Samia Suluhu Hassan mjini Geita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here