Waziri wa Fedha atoa wito kwa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB)

DOHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) ametoa wito kwa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) kuimarisha zaidi ushirikiano na wanachama wake ili kuboresha maendeleo ya miundombinu itakayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu.
Mhe. Balozi Omar ametoa rai hiyo wakati akichangia mada kwenye mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki hiyo wa mwaka 2026, uliofanyika katika hoteli ya Sheraton, Doha nchini Qatar.

Alisisitiza kuwa AIIB inapaswa kushiriki mapema katika hatua za utambuzi na uwekaji vipaumbele vya miradi mikubwa ya kitaifa katika nchi wanachama wa Taasisi hiyo yenye Makao yake Makuu Beijing nchini China.
"AIB itoe msaada wa kiufundi na kifedha ili kuhakikisha miradi inakuwa na tija, inakidhi viwango vya kiufundi, na iko tayari kutekelezwa ili kupunguza pengo la miundombinu katika nchi wanachama, huku ikizingatia tofauti za kimaendeleo kati ya eneo na eneo,” alisema Mhe. Balozi Omar.
Katika Mkutano huo, AIIB imewaleta pamoja serikali, washirika wa maendeleo, na wawekezaji binafsi ili kuchochea uwekezaji katika miradi ya kimkakati. Uhamasishaji wa mitaji binafsi ili kuboresha miundombinu ikiwemo nishati ya umeme, migumo ya kidigitali, reli na miradi mingine inayohusiana na hifadhi ya mazingira.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here