DOHA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amewasili Doha nchini Qatar kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia (AIIB) unaofanyika Septemba 28 hadi 29, 2026 mjini Doha, Qatar.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Doha-Hamad, Mhe. Balozi Omar, alipokelewa na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar, Bi. Maryam Haji Mrisho, kwa niaba ya Balozi , Mheshimiwa Habibu Awesi Mohamed.Mkutano wa Mwaka wa AIIB, unawakutanisha viongozi wa serikali, watunga sera, na wadau wa kibiashara kujadili mustakabali wa uwekezaji endelevu wa miundombinu, ambapo Tanzania ni Mwanahisa wa Taasisi hiyo yenye Makao yake Makuu nchini China.

