Dkt.Yonazi atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki

ANKARA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu,Dkt. Jim Yonazi ameupongeza Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uturuki kwa kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kidiplomasia, biashara, uwekezaji, na maendeleo ya kijamii.
Dkt.Yonazi ametoa pongezi hizo alipotembelea Ofisi za Ubalozi huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mjini Ankara, Uturuki iliyolenga kuimarisha uwezo wa kitaasisi, kuongeza maarifa ya kiufundi na kukuza ushirikiano katika kupunguza vihatarishi vya maafa, kukabiliana na dharura na mifumo ya kurejesha hali kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kiteknolojia.

Dkt. Yonazi amesema kuwa,ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki unazidi kuimarika kwa kasi kubwa, ukiongozwa na diplomasia ya kiuchumi, miongozo ya kimkakati kama vile Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ya Tanzania, pamoja na ziara za kitaifa za viongozi wakuu wa nchi hizo mbili.
Naye Kaimu Balozi,Bi. Levina Maleo ambaye ni Mkuu wa Utawala wa ubalozi amempongeza na kumshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea ofisi za Ubalozi na kueleza kuwa wataendeleza mashirikiano yaliyopo kati ya nchi hizo mbili na kuendelea kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa za elimu, afya na kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here