Soma habari zote muhimu leo Oktoba 18, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, HabariLeo, Majira, Nipashe, Zanzibar Leo, Raia Mwema, Mwanahalisi, Uhuru, Pambazuko, Jamhuri na mengineyo kila siku bila malipo.
Gazeti la Habarileo leo Jumapili, Oktoba 18, 2026 ukurasa wa mbele, habari kubwa ni Marekani yalegeza tahadhari ya usafiri Tanzania, pia Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi ‘kuwavaa’ watendaji wazembe baada ya kubaini maagizo yake hayajatekelezwa.
Gazeti la Mwananchi leo Jumapili Oktoba 18, 2026, ukurasa wa mbele vichwa vilivyopewa uzito ni Simu za mkopo zilivyo mateso, Wanakijiji waingia mkenge kwa kuunganishiwa umeme na vishoka, , Bwawa la Nyerere laongeza mapato mara sita Tanesco, Vyama 13 DRC vyafungiwa kwa kumuunga mkono Kabila, na Ripoti ya wizi wa pikipiki, mifugo, uvunjaji waongoza.
Gazeti la Nyakati leo Jumapili, Oktoba 18-24, 2026 linaangazia ukurasa wa mbele kuwa, Papa Leo agundulika kuwa na Saratani na kufanyiwa upasuaji wa haraka kuondoa sehemu ya pafu, na Ziara ya Waziri Mkuu wa Israeli huko Uarabuni yaikera Iran.Gazeti la Mzalendo leo Jumapili Oktoba 18-24, 2026 linaangazia ukurasa wa mbele kuwa Ndejembi akunjua makucha, na CCM yaagiza kukamilika Daraja Muhoro.
Gazeti la Zanzibar leo Jumapili Oktoba 18, 2026 linaangazia ukurasa wa mbele kuwa Dk. Mwinyi atoa wito mataifa kufadhili miradi uhifadhi bioanui, na Mazrui ataka Chuo cha Afya kirudishwe Wizara husika.







