DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 1, 2026 amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
Walioapishwa ni Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera kuwa Waziri wa Nishati; na Mhe. Masanja Kungu Kadogosa kuwa Waziri wa Ujenzi.
Halikadhalika, Rais Dkt. Samia amemuapisha Bi. Asha Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, anayeshughulikia masuala ya usimamizi wa fedha.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.
