DAR ES SALAAM- Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza mabadiliko katika kalenda ya minada ya Dhamana za Serikali kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/27.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 5, 2026 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Benki Kuu itaendesha minada ya Dhamana za Serikali za muda mfupi za siku 35, 91, 182 na 364, pamoja na Dhamana za Muda Mrefu (Hatifungani) za miaka 2, 5, 10, 15, 20 na 25 katika robo hiyo.
Kiwango cha riba kwa Hatifungani pamoja na taarifa zaidi za dhamana husika zitatangazwa kwenye tangazo la mnada (Call for Tender).
Kalenda ya minada ni kama ifuatavyo:
