Soma habari zote muhimu leo Jumatano Novemba 4, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, Majira, HabariLeo, Nipashe, Zanzibar Leo, Mwanaspoti na mengineyo kila siku bila malipo.
Gazeti la Raia Mwema, Jumatano, Novemba 4-10, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Lissu: Nitamzika Kaka, Maajabu ya Mji Serikali Mtumba na Lema moto - Hoja zake zaibua mjadala mzito.Gazeti la Majira, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Serikali yazidi kuimarisha huduma za mawasiliano, Tume ya Haki za Binadamu kuimarisha upatikanaji haki na Polisi yaonya wanaopanga vurugu hukumu ya Lissu. Ukurasa wa michezo: Kocha Simba awapa tano wachezaji wake.
Gazeti la Nipashe, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Lema, CHADEMA bado hakujatulia, LAAC yahoji bilioni 120/- za mikopo ya 10%, Matokeo la 7: nyuma ya pazia watahiniwa kuandika matusi, hukumu kesi ya lissu yageuka mtihani polisi, minara 2,000 yawafungulia mawasiliano watanzania milioni 32, kombo akutana na mfalme charles III, na miaka 34 ya mbowe kisiasa hadi kugeukia ujenzi wa makanisa.Ukurasa wa michezo: mjerumani, yanga sasa kimeeleweka, barker: haikuwa rahisi, na jkt yatamba kuisimamisha simba sc.
Gazeti la Mwananchi, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Msigwa amtega Lema, Kamati tatu za Bunge zaibua madudu, Mradi wa umemejua Bambi kuanza majaribio, Wanafunzi 371 kurudia mtihani darasa la saba, na Samuel Sitta na kipimo cha juu viwango bungeni.
Gazeti la Mwana Spoti, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Tishio Simba liko hapa, Yanga imeanza, Simba imefuata Nov 29, Kuna shida matumizi ya Fvs, na Mchezaji aliyezimia uwanjani afariki.Mechi kubwa za Uefa Leo: Rb Leipzig vs Man City saa 5:00 usiku Red Bull Arena, Slavia Praha vs Arsenal saa 3:00 usiku, na Fenerbahce vs Liverpool.
Gazeti la Uhuru, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Ufaulu waliomaliza elimu msingi wapaa, Wavulana waibuka vinara, masomo ya Kiswahili na Hisabati yaongoza, 429,667 wapata madaraja A na B, Watahiniwa 371 washindwa kufanya mtihani kwa maradhi, Sababu 6 chanzo bilioni 120.48/- kutorejeshwa, Serikali kuendelea kumuenzi Samuel Sitta, Ucsaf kufikisha huduma ya mawasiliano Sgr, Tazara, na Wapigakura 133,864 kuchagua mrithi wa Ndejembi Chamwino.
Ukurasa wa michezo: Rekodi kabambe Simba, Kocha Barker ni shangwe tu, Man U yapiga panga, Tanzania, Djibout hapatoshi, na Arsenal yampigia hesabu Yildiz.
Gazeti la Taifa Tanzania, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Chadema wawashtukia wanaharakati, Mjadala wa Lema kuwashutumu Mange na Maria Sarungi wapoozesha hukumu ya Lissu, Khalfan Milongia atupwa jela maisha kwa kosa la kubaka mtoto, Necta kuchunguza shule 13 zilizopata daraja E, Ucsaf yaelekeza nguvu Halmashauri na Kata zote nchini, na Pic yanyooshea kidole mashirika yanayoitia hasara serikali.
Ukurasa wa michezo: Barker: Namungo Fc walitaka kutuangusha, lakini tukapambana, Mshambuliaji Jesus De Miguel afariki dunia baada ya rafu mbaya, Azim Dewji awachapa wanaodai hisa Simba, na Tamasha la Tanzania Comedy kufanyika Novemba 27.
Gazeti la Tanzania Leo, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Samia aendeleza rekodi ya uchumi, Tanzania kuvutia uwekezaji mkubwa wa nishati duniani, Mabenki yaogelea kwenye faida ya karibu tril. 2/-, Tasac yakoshwa na uwekezaji Dp World bandari ya Dar, Lindi, Mtwara kuunganishwa gridi ya taifa ya umeme, Ufaulu darasa la saba wapanda hadi 85.22%, na Polisi yaonya wanaohamasisha vurugu Nov. 6.
Ukurasa wa michezo: Barker ashtukia jambo, awapa onyo mastaa Simba Sc, Pacome aibua mapya Yanga Sc, Damaro aukana uraia, atimka Singida Bs, Mzungu wa Singida Bs avunja mkataba, na Los Angeles Lakers yaifumua Miami Heat.
Gazeti la Habari Leo, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Bunge lacharuka, Laagiza mashirika yote yachangie Mfuko Mkuu wa Serikali, yazitaka bil 37/- za halmashauri, Lataka mikataba Brt ipitiwe upya, Nhif ikusanye bil 104/-, Trilioni 40/- kujenga barabara nne za kimkakati, Tra yaagizwa kuchukulia hatua walipakodi 17,573, Ucsaf yawezesha mawasiliano wananchi mil 33, Padri, wenzake 8 wana kesi ya kujibu mauaji ya mtoto Albino, na Watu watatu wafa ajalini Mtwara.
Ukurasa wa michezo: Wachezaji Simba wamkosa Barker, Frat yamsimamisha Katibu Mkuu Mapunda, Taifa Stars kuinoa kuivaa Nigeria, na City kicheko Singida kilio.
Gazeti la Mwelekeo, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Lema avuruga Chadema, Hoja za Lema zagawa vigogo, wanachama na Suala maridhiano lageuka mwiba ndani ya chama.
Ukurasa wa michezo: Tatizo Simba SC ni Mangungu, MO au Magori?.
Gazeti la MwanaHabari, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Tanzania yatumia mkutano mkuu ISA kuvutia uwekezaji, Ufaulu la saba waongezeka kwa asilimia 3.4 na Mkenda aitaka COSTECH kuhakikisha tafiti, ubunifu vinafika sokoni.
Gazeti la Wamachinga, Jumatano, Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: Ufaulu la saba wapaa ni kwa asilimia 85.22, Malisa akabidhi ofisi, amuomba Rais Samia radhi na Ndejembi amchambua Hayati Sitta alivyoacha, kuishi dira ya uongozi.
Gazeti la Sauti Yetu, Jumatano Novemba 4, 2026 habari kuu zilizopewa kipaumbele ni: PIC yawaslisha mapendekezo 12 - Ni ya kuimarisha uwekezaji wa mitaji ya umma, Hoja za wanaharakati, Lema apumua - Wataka maamuzi ya vikao viheshimiwe, ACT Wazalendo yalia na maisha magumu kwa wananchi, na SERIKALI YAIMARISHA MIKAKATI KUPUNGUZA UDUMAVU.
Gazeti la Mtanzania Leo, Jumatano Novemba 4, 2026 habari kuu ni: UCSAF yawafikia watu milioni 32 - Yajenga minara 758 kwa shilingi bilioni 126, TRA yasifu mchango wa viwanda, biashara ndogo na za kati, Wasichana waongoza matokeo darasa la saba, ufaulu waongezeka, na Tanzania yatumia mkutano wa ISA India kuvutia uwekezaji mwanga wa jua.
Gazeti la Dira ya Mtanzania, Jumatano Novemba 4, 2026 habari kuu ni: Lema mwamba mgumu Chadema - Azidi kuungwa mkono, Chadema wazidi kupagawika, UFAULU WA DARASA LA SABA WAFIKIA ASILIMIA 85.22, PIC yatoa onyo - Yataka thamani ya hisa iendane na gawio, na UCSAF yajenga minara 758 ya bilioni 126, wananchi milioni 8.5 kunufaika.
Gazeti la Biashara Leo, Jumatano Novemba 4, 2026 habari kuu ni: Rais Samia afikisha mawasiliano vijijini - Mamilioni sasa wanafaidi mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), na Ofisi ya Msajili wa Hazina yataka wahariri watoe elimu mchango wa mashirika ya umma.Gazeti la Mwananchi Huru, Jumatano Novemba 4, 2026 habari kuu ni: UCSAF yajipanga kuwapa raha abiria treni ya SGR - Yaahidi kuhakikisha mawasiliano yanapatikana muda wote safarini, RC Tabora aliyetumbuliwa amwomba radhi Rais Samia, TRA yahimiza wananchi kulipa kodi kwa hiyari, na Baraza la Wafanyakazi TEA lapitia mpango mkakati wa tano.
















