Kamati ya Bunge yataka mazingira yalindwe kwa wivu mkubwa

MOROGORO- Viongozi wa Serikali wametakiwa kuwashirikisha wananchi katika ulinzi na uendelezaji wa vyanzo vya maji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) amesema hayo Novemba 8, 2026 wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Mheshimiwa Kiswaga akiongoza kamati hiyo katika ziara ya kikazi kukagua utetekelezaji wa miradi ya maji ameainisha kuwa, utunzaji wa vyanzo vya maji ni lazima kwa uendelevu wa miradi ya maji na maisha ya sasa na baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Wakili Dunstan Kyobya akiipokea kamati hiyo ofisini kwake amesema, Serikali inapokea maelekezo ya kamati na inafanya kazi saa 24 kulinda mazingira na kutoa suluhu kwa changamoto zunazoibuka ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Amesema, uwepo wa kamati katika Wilaya ya Kilombero ni fursa ya kufanya vizuri zaidi katika utunzaji na uendelezaji wa rasilimali za maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here