Waziri Homera ampongeza Rais Samia kuongoza kwa vitendo ajenda ya nishati safi ya kupikia Afrika

📌Ataja matumizi ya nishati safi kupanda kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 28.6 mwaka 2025

📌Wizara kuja na mkakati kabambe wa kuwawezesha vijana kutengeneza majiko banifu nchi nzima

📌TANESCO,REA na TPDC kuongeza kasi ya utoaji elimu na usambazaji wa majiko banifu na ya umeme

ANTALYA- Waziri wa Nishati, Mhe Juma Homera, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuongoza jitihada za kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini, akisema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza ajenda hiyo barani Afrika.
Waziri Homera alitoa pongezi hizo tarehe 11 Novemba wakati akitoa salamu za ukaribisho za Wizara ya Nishati kwa Rais Samia katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kutangaza mafanikio ya mpito wa Nishati Tanzania na Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Shule na Vituo vya Afya, uliofanyika pembezoni mwa COP31 jijini Antalya, Türkiye.
Alieleza kuwa, chini ya uongozi wa Rais Samia, matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini yameongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 28.6 mwaka 2025, hatua inayoonesha maendeleo katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia wa 2024–2034.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo na taasisi za kimataifa kujadili mafanikio, fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano katika kuharakisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Tanzania inalenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here