Mheshimiwa Salome atoa siku tano kwa ETDCO kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Kuboresha Hali ya Umeme (AVR) Nanyumbu

MTWARA- Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, ameiagiza kampuni tanzu ya TANESCO ya ETDCO kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Kuboresha Hali ya Umeme (AVR) kilichopo Mangaka, Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, ambacho kitaongeza nguvu ya kuendesha mradi wa maji na hivyo kuwawezesha wananchi kupata maji kwa ufanisi.
Kituo hicho cha AVR kinajengwa kwa lengo la kuimarisha kiwango cha volteji ya umeme unaosambazwa katika mradi wa maji wa Mangaka, hatua itakayosaidia mitambo ya kusukuma maji kufanya kazi kwa ufanisi na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Mhe. Salome ametoa agizo hilo leo, Novemba 12, 2026, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho unaotekelezwa na Kampuni ya ETDCO.
Amesisitiza kuwa, kazi zote zilizosalia zinapaswa kukamilishwa ndani ya muda alioutoa ili kituo hicho kianze kufanya kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here