BREAKING NEWS: Bernad Membe kuelezea kinachomsibu saa chache zijazo

HABARI zilizotufikia muda huu ni kwamba mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard K.Membe anataraja kufanya mkutano na waandishi wa habari saa chache zijazo.

Duru za habari kutoka mjini mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu zimeieleza Diramakini kuwa, mchana wa leo akitua uwanja wa ndege atazungumzia yanayomsibu na hatua itakayofuata.

"Kwa sasa yupo sawa,  afya yake imeimarika, pengine usubirie akifika mchana ili uweze kumuhoji hayo unayotaka kuyafahamu. Ila maandalizi ya kuondoka hapa Dubai yamekamilika na saa nane atazungumza.

"Hiyo press conference ni muhimu sana, itafanyikia pale Airport, ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa, afya imeimarika na kampeni zitaendelea kama kawaida pengine zitaanzia Ukanda wa Magharibi,"duru za habari zimeidokeza Diramakini kutoka mjini Dubai.


No comments

Powered by Blogger.