BREAKING NEWS: Ndege ya jeshi yaua 22

Ndege ya abiria ya Jeshi aina ya Antonov An-26 (turboprop) ambayo ilikuwa imebeba watu 28 inaripotiwa kuanguka mjini Kharkov Kaskazini Mashariki mwa Ukraine na kuua watu 22.

(Idara ya Dharura/AP).
Watu wengine wawili wamejeruhiwa vibaya na wengine wanne bado hawajulikani waliko, Wizara ya Mambo ya Ndani imebainisha kupitia taarifa yake. Unaweza kuisoma hapa kwa kina.

Ajali hiyo ilitokea majira ya leo saa 20:50 kwa saa za huko (19:50 CET) karibu na mji wa Mashariki wa Chuhuyiv, katika Mkoa wa Kharkiv, umbali wa kilomita mbili kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi.

Watu 28 waliokuwemo ndani ya ndege ya AN-26 walikuwa marubani wa kijeshi na maafisa wa Chuo Kikuu cha Kikosi cha Anga cha Kozhedub. Awali wizara ilikuwa imesema kuwa watu 24 walikuwa kwenye ndege wakati ikianguka.

No comments

Powered by Blogger.