Iran:Makubaliano hayawezi kudumu hadi tudhibiti siasa za Kibeberu

JAMHURI ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa, makubaliano yoyote ya Kimataifa hayawezi kudumu bila kuwepo uwiano sawa wa haki, maamuzi na hatua za kiutekelezaji.
Naibu Waziri,Mohsen Baharvand.(IRNA).

Mohsen Baharvand ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya haki za kimataifa amesema hayo.

Amesema, makubaliano yoyote yale ya kimataifa hayawezi kudumu bila ya kuwepo mlingano sawa katika utekelezaji wa haki na majukumu, na kwamba mapatano ya nyuklia ya JCPOA nayo hayawezi kutoka kwenye msingi huo.

Baharvand ameyasema hayo jana Jumatano katika kikao cha Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) mjini Vienna,Austria.

Naibu Waziri huyo amebainisha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu mapatano hayo ya nyuklia.

Amesema,isitarajiwe kwamba Iran itekeleza majukumu yake yote ndani ya JCPOA bila  kupata haki zake zilizoainishwa kwenye makubaliano.

" Je, JCPOA na ukaguzi unaofanywa na IAEA nchini Iran kwa mujibu wa mapatano ya JCPOA ni mambo ambayo yataendelea hivi hivi? Alihoji na kujibu kuwa ni ndiyo, lakini kwa sharti kwamba wajumbe wa jamii ya kimataifa wasimame imara kukabiliana na siasa za kibeberu za Marekani na wachunge thamani, mambo muhimu na haki za mataifa yote,"amesema.

No comments

Powered by Blogger.