JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAARIFA FUPI YA KITAKWIMU KUHUSU MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO JUU YA UKUAJI WA UCHUMI NA UBORESHAJI WA MAISHA YA WATANZANIA

Mwenendo wa Uchumi Katika Awamu za Serikali Katika miaka mitano iliyopita, kwa mujibu wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Tanzania imepata mafanikio makubwa kiuchumi kutokana na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. 

Uchumi umeendelea kukua kwa kasi ya wastani wa asilimia 6.9 kwa miaka mitano iliyopita, ikiwa ni ukuaji mkubwa zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika ambayo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi. 

Kutokana na ukuaji huo, Benki ya Dunia iliitangaza Tanzania kuwa nchi ya kipato cha katimwaka 2019.

 Jedwali Na. 1 juu linaonesha viashiria mbalimbali vya uchumi kwa Awamu zote Tano za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kwa ujumla, katika miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano, imefanikiwa kukuza uchumi wa nchi kwa kasi kubwa zaidi ikilinganishwa na Awamu Nne zilizopitaambazo zimeongoza Serikali kwa miaka kumi.

No comments

Powered by Blogger.