Kamati: Viongozi wa dini acheni kabisa, hii tabia haikubaliki, madhabahu hazipaswi kuingiliwa kisiasa

Kamati ya Amani imelaani vikali vitendo vya baadhi ya viongozi wa dini kutumia madhabahu na nyumba za ibada kufanya kampeni za kuwanadi wanasiasa jambo ambalo ni kinyume na maadili.Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema, kama vitendo hivyo vitafumbiwa macho vinaweza kuhatarisha hali ya amani na kuwagawanya waumini wanaokwenda kusali.

Aidha,amesema kama kiongozi wa dini anaona mgombea fulani anamfaa ni vyema akaenda kwenye majukwaa ya siasa ili kumnadi, lakini sio kutumia nyumba za ibada kunadi wanasiasa.

Katika mkutano huo pia umehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Amani wakiwemo maaskofu, manabii, wachungaji, maimamu na masheikh ambapo wote kwa pamoja wamaonyesha kutokufurahishwa na vitendo hivyo katika nyumba za ibada.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news