Maalim Seif aomba kura aweze kwenda kukubaliana upya mambo ya Muungano

Mgombea urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema endapo wananchi watampatia ridhaa ya kumuweka madarakani ataunda Jeshi la Polisi la Zanzibar pia atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano kujadili upya mambo ya Muungano, anaripoti Talib Ussi (Diramakini) Zanzibar. 

Maalim Seif ameyaeleza hayo huko Mkoa wa Kusini Pemba katika Jimbo la Kiwani katika muendelezo wa kampeni zake za urais.

Amesema, wakati huu wa vuguvugu la siasa imekuwa ni kawada viongozi wao kukamata, lakini wakifika kituoni huhojiwa na askari kutoka Tanzania Bara na kudai hilo litafika mwisho kwani akipata ridhaa ataunda Jeshi la Polisi Zanzibar.

Amesema, Zanzibar kukosa Jeshi la Polisi, vijana wengi wamekuwa wakikosa ajira kwa sababu wanaonekana wapinzani.

“Nitaanzisha jeshi letu wenyewe hapa na Zanzibar itakuwa na mamlaka kamili ya kutenda tunalolitaka,"amesema Maalim Seif.

Sambamba na hilo Maalim Seif amesema kwa upande wa Muungano mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais atazungumza na Rais wa Jamuhuri kukubaliana upya kuhusu mambo ya Muungano.

Amesema, kwa sasa wananchi wa Zanzibar wanaonekana si raia kutokana na nchi yao kukosa utambulisho wa Dunia.
Mgombea wa Urais Kupitia Chama Cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa Majimbo ya Kiwani na Chambani katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mauwani Kiwani Mkoa wa Kusini  Pemba. (Diramakini).

Pia Maalim Seif amesema kuwa, atahakikisha anairudisha Benki Kuu ya Zanzibar ili waweze kudhibiti fedha zao.

Maalim Seif amesema kuwa, katika Serikali yake wazee watalipwa zaidi ya shilingi laki moja kwa mwezi ili na wao watumie maendeleo vizuri ya nchi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news