Marehemu Mzee Saidi Mabera wa Msondo Ngoma Music Band aacha simanzi

Usiku wa kuamkia leo Septemba 29,2020 mwanamziki mahiri, mpiga gitaa Mzee Saidi Mabera amefariki dunia.

Mzee Saidi Mabera alikuwa mwanamuziki wa bendi kongwe barani Afrika ya Msondo Ngoma Music band yenye makao yake nchi Tanzania.

Marehemu alijiunga na bendi hiyo mwaka 1973 na hajawahi kuhama, ndiye mwanamziki pekee mkongwe nchini Tanzania aliyeweka rekodi ya kutulia katika bendi moja bila kuhama.

Marehemu Saidi Mabera atakumbukwa daima katika mchango wake kimuziki na ustadi wake wa upigaji wa gitaa la solo.

                                                         SERIKALI YAOMBOLEZANo comments

Powered by Blogger.