Mgombea Ubunge CCM afariki ghafla usiku huu

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar na mgombea wa sasa, Salim Turky amefariki dunia.

Mgombea huyo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeieleza Diramakini kuwa, amefariki dunia usiku huu katika Hospitali ya Global baada ya kuugua ghafla.

Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mbunge wa Jimbo la Mpendae tangu 2010, alizaliwa Februari 11, 1963. 

Hadi umauti unamkuta alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya Turky ambapo chini yake yalikuwa makampuni 12 yanayoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na visiwa vya Comoro.

Baadhi ya makampuni hayo yanajumuisha hoteli ya Golden Tulip, hospitali kubwa ya Tasakhtaa Zanzibar, pia ilijihusisha na biashara ya saruji, Nitak communications, vyakula na mafuta.

Turks Group iliazishwa mwaka 1978 kama duka la nguo na ndugu wa familia moja ambao ni Salim, Murtadha na marehemu Yunus pamoja na baba yao, Hassan Turky na miaka 40 baadae wakalibadilisha kuwa moja ya makampuni yanayoongoza Tanzania.

Mwaka 2017,Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, Salim Turky alitafuta ndege iliyompeleka Lissu Nairobi na kuwa mdhamana wa deni la kukodi ndege iliyokuwa inamilikiwa na FlyghtLink ambao ni jamaa zake katika biashara. 

Uongozi wa Diramakini Business Limited unatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na CCM kwa kuondokewa na mpendwa wao, Mwenyenzi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema.

Kwa taarifa zaidi kuhusu tanzia hii fuatilia Diramakini tutakujuza yote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news