Polepole: Nasikia 'wamemla kichwa'

"Huyu anasema atarasimisha kangomba. Amepewa dhamana ya kimataifa kwa miaka 8 haelewi kangomba ni nini. Nasikia wamemla kichwa. Sisi tumefurahi sana. Hawa wasisubiri tarehe 3, waungane now (sasa), tutawaonesha sisi ni akina nani,"amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole wakati akielezea kuhusiana na tathimini ya kampeni zao leo Septemba 25, 2020 jijini Dodoma.

Pia amesema kuwa, katika miaka mitano ya Rais Dkt,John Magufuli pato la Taifa limeongezeka na limefikia hatua kubwa katika maendeleo.


“Katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt. John Magufuli, pato la taifa ni shilingi trilioni 124 kwa mwaka. Hii ni hatua kubwa katika maendeleo.Tumeboresha huduma za reli ya kati ili kusaidia abiria kusafirisha mizigo yao, tumeongeza uzito wa reli hiyo ya kati ambapo sasa itakuwa na ratili 70 hadi 80 na itakuwa na uwezo wa kutembea 70km hadi 80km kwa saa. Hii ni tofauti kubwa ukilinganisha na mwendo wa 15km kwa saa kabla ya 2015.”

“Kwa dhati tunampongeza mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi, Dkt John Magufuli kwa kufanya kampeni kistaarabu kwa kuzungumza hoja, sera na yaliyoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya 2020. Majukwaa ya kampeni yanapaswa kutumika kistaarabu.

“Kampeni zinaendelea vizuri huko Zanzibar. Mwitikio wa Wazanzibar katika kampeni za mgombea urais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi umetupa deni kubwa la kuwapatia maendeleo wananchi.

“Tunatambua kwa dhati mchango wa viongozi wa dini, dua zenu na maombi yenu yametufanya tuendelee kuimarika. Mgombea wetu ameendelea kuwa na afya imara kwa sababu ya maombi yenu,"amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news