RAIS DOKTA JOHN MAGUFULI: Geita! Geita! Geita! Geita! Geita!, Asanteni! Asanteni! Asanteni! Asanteni! Asanteni!


Sehemu ya maelfu ya wananchi wa Katoro na Buseresere wakishangilia wakati Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili Katoro mkoani Geita.

"Upendo wenu unanipa tafakari kubwa mno, nakosa cha kusema ila sitawaangusha kamwe"

Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Wananchi wa Katoro katika mkutano wa Kampeni za CCM wakati akielekea Chato mkoani Geita leo tarehe 9 Septemba 2020.


Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa na pacha wake Kurwa Biteko pamoja na wagombea Ubunge wengine wa CCM mkoa Geita.

Sehemu ya maelfu ya wananchi wa Katoro na Buseresere wakishangilia wakati Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili Katoro mkoani Geita. (Saa 24 wasiliana nasi diramakini@gmail.com). 

Akiwahutubia maelfu ya wananchi hao, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema, Geita licha ya kunufaka na madini, imekuwa na eneo la utalii, ndiyo maana imeanzishwa hifadhi ya Burigi Chato ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini. 

Hifadhi hiyo kama zilivyo nyingine hapa nchini licha ya kusaidia uhifadhi wa mazingira kwa ajli ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Rais amesisitiza hiyo ni fursa kubwa kwa wananchi na wakazi wa Geita kuharakisha maendeleo yao, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Amesema, Serikali yake inataka kila kanda kuwepo na utalii, "zamani ilikuwa utalii ni Kaskazini tu, lakini sasa tumeamua na tutakuwa tunaanzisha hifadhi katika maeneo mbalimbali nchini kwetu.Kila mahali kuwepo na hifadhi za taifa za utalii, ndio maana tunajenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwanza ili watalii wakija wanavuka daraja la Busisi, wanakuja na huku.

"Tuanze kuchangamkia fursa, watu waanze kujenga nyumba za kulala wageni kwa ajili ya watalii.Tunataka fedha ambazo zinatokana na utalii ziongezeke, hata hili Ziwa Victoria ni utalii na kwa kuendelea kufungua milango ya utalii nchini kwetu tunaamini tutaweza kuleta maendeleo makubwa mno,"Rais Dokta Magufuli amewaeleza wananchi hao maelfu kwa maelfu.

Pia mgombea urais huyo ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelezea kuhusiana na kilimo, uvuvi na ufugaji ambapo amesema wametoa kipaumbele kikubwa kuendelea sekta hiyo.

Amesema, lengo la kufanya hivyo wanataka wakulima , wafugaji na wavuvi nao wafaide huku akieleza katika kipindi cha miaka mitano kuna hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa na zimeleta matokeo makubwa kwa makundi hayo nchini. 

Dokta Magufuli amesema, upo mkakati kabambe wa kujengwa kwa machinjio ya kisasa ya nyama mkoani Geita.

Mradi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni saba unalenga kuwezesha uchinjaji nyama kwa matumizi ya ndani na kuvungashwa kwa ajili ya kuuza nje, vivyo hivyo sekta za kilimo na uvuvi Ilani ya Uchaguzi 2020 hadi 2025 imetoa maelekezo ambayo ni ya neema kwa makundi hayo na anaamini baada ya Oktoba 28, mwaka huu watafurahia matunda yake.

Rais Magufuli amesema pia katika kipindi cha miaka mitano barabara za lami zenye urefu wa kilomita 123.23 zimejengwa na wananchi wa mkoa huo ni mashahidi, kwani hata mji huo haukuwa na barabara za lami kama ilivyo sasa.  

"Kuna babarabara ya Nyahunga -Ushilombo yenye urefu wa kilomita 52, tumejitahidi kujenga barabara za lami na tutaendelea na tumepanga barabara ya Geita kwenda Kahama itajengwa kwa kiwango cha lami pia, hivyo miaka mingine ijayo tutafanya zaidi,naombeni kura zenu zote,"amesema.

Pia amesema mafanikio yaliyopatikana mkoani humo katika kipindi hiki kinachomalizika miaka mitano katika sekta ya afya, elimu, miradi ya maji, nishati na nyingine watarajie makubwa zaidi kwani safari waliyotoka ilikuwa mbali, lakini sasa mwendo wa kufika mbali wakiwa na mambo mazuri katika nyanja mbalimbali utaanza baada ya Oktoba 28,mwaka huu kwa utekelezaji zaidi.(Saa 24 wasiliana nasi diramakini@gmail.com).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news